Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lindelof ashinda tuzo ya beki bora Sweden

D6F0D366 D373 4A21 9116 11382F276706.jpeg Beki wa Man United, Victor Lindelof

Mon, 26 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa kati wa klabu ya Manchester United Victor Lindelof amechaguliwa kua beki bora wa mwaka nchini kwao Sweeden kwa mara ya nne mfululizo.

Beki huyo anayekipiga katika klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Sweeden amechaguliwa na Shirikisho la soka nchini humo kama beki aliecheza kwa kiwango bora zaidi kwa msimu uliomalizika kutoka nchini humo.

Victor Lindelof anafanikiwa kushinda tuzo hiyo kwa mara ya nne mfululizo huku kwa ujumla akiwa amefanikiwa kubeba tuzo hiyo mara tano, Beki huyo amefanikiwa kushinda tuzo hiyo kutokana na kiwango ambacho amekua akionesha kwenye timu ya taifa ya nchi hiyo pamoja na klabu yake ya Manchester United.

Victor Lindelof ambaye alisajiliwa ndani ya klabu ya Manchester United mwaka 2017 chini ya kocha Jose Mourinho amekua akipata nafasi ya kucheza kwa muda mrefu tangu ajiunge klabuni hapo, Lakini kwasasa ameonekana kukosa nafasi ya kuanza mara kwa mara tangu kocha mpya wa klabu hiyo Erik Ten Hag ajiunge na mashetani hao wekundu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live