Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ligue 1 ukizingua tu, ndo basi tena

PSG Leo Ligue 1 ukizingua tu, ndo basi tena

Sat, 11 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wikiendi hii Ligi Kuu Ufaransa itakuwa katika mzunguko wa 33, ambapo kila timu itakuwa ikicheza mechi ya hatua hiyo kasoro nne ambazo zina viporo zitakazokuwa zinacheza mechi za 32.

Viporo vya timu hizo nne ambazo ni PSG, Nice, Reims na Marseille vitachezwa katikati ya wiki ijayo na baada ya hapo kila timu itakuwa imebakisha mchezo mmoja ili kumaliza ligi.

Kwa ujumla ligi itaisha Mei 19, ambapo timu 18 zitashuka uwanjani kukamilisha ratiba ingawa wiki hii ndio itatoa majibu ya maswali mengi juu ya vita zinazoendelea katika msimamo.

Timu ambayo itapoteza wikiendi hii itakuwa imejiweka kwenye mazingira magumu kuliko kawaida katika kile inachokipambania.

Kule chini timu ya kwanza ambayo ikifungwa inakuwa imeshajiondoa katika ligi ni Clermont inayocheza na Lorient, kiujumla timnu hii ina alama 25, hivyo ikipoteza itashuka kwani hata ikishinda mechi ya mwisho haitoweza kufikia alama za Metz yenye pointi 29 ikiwa katika eneo la kucheza mtoano ili kubaki.

Ubaya ni kwamba mechi hiyo inawakutanisha wote wanaoshika nafasi mbili za mwisho, Clermont ikiwa ya 18 na Lorient 17.

Ikiwa Lorient itapoteza mechi hii itakuwa inasubiria maajabu Metz iliyopo juu yake nayo ifungwe, lakini mambo yakienda tofauti Metz ikapata hata sare basi rasmi Lorient itakuwa imejishusha.

Hii ni sawa na ilivyo kwa Metz na Le Havre ambapo ikiwa Metz itapoteza mechi ya wikiendi hii itakuwa inaiombea Le Havre nayo ifungwe kwani ikipata hata sare, wao(Metz), watatakiwa kucheza mechi ya mtoano ili kubaki katika ligi hata kama watashinda mchezo wao wa mwisho wa ligi.

Kwa upande wa juu, Rennes inayopambana ili kufuzu walau michuano yoyote ya Ulaya, ikiwa itafungwa na Reims itakuwa imejiondoa rasmi kufuzu.

Kwa sasa Rennes ina alama 45 ikiwa katika nafasi ya nane huku Olympique Lyon inayoifuatia inashikilia nafasi ya saba kwa pointi 47, lakini timu ambayo ipo katika eneo la kufuzu michuano ya Conference League, Lens ina pointi 49, hivyo Rennes ikipoteza hata ikishinda mchezo wao wa mwisho haitoweza kufikia alama za Lens.

Vilevile Lyon kama ikifungwa na Lens ikashinda basi itakuwa imejiondoa katika nafasi ya kufuzu michuano ya Ulaya.

Chanzo: Mwanaspoti