Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#LigiKuu: Orodha ya makipa wanaoongoza kwa cleansheets mpaka sasa

Diarra Na Manula .jpeg Djigui Diarra na Aishi Manula

Sun, 5 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchuano ni mkali wa cleanaheets kwa magolikipa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo mpaka sasa kipa namba moja wa Yanga, Djigui Diarra anaongoza orodha akiwa hajafungwa katika mechi 13.

Manula ambaye ni kipa namba moja wa Timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) amekuwa na kiwango kizuri sana takribani miaka yote ya uchezaji wake toka akiwa Azam na sasa akiwa Simba.

Pia golikipa huyo amechukua tuzo za golikipa bora mara tano mfululizo, japokuwa msimu uliopita alipitwa na mlinda mlango wa Yanga Djigui Diara raia wa Mali.

Diarra bado cleansheets mbili (2) avunje rekodi yake mwenyewe ya msimu uliopita (2021-2022) ambapo alikuwa na cleanshees 15 katika mechi 24 alizocheza za ligi.

Hii hapa orodha ya magolikipa wanaoongoza kwa kucheza mechi nyingi bila kuruhusu goli langoni mwao (clean sheets) hadi kufikia mzunguzo wa 22 wa Ligi Kuu Tanzania Bara (Februari 4, 2023).

1:Djigui Diarra – Yanga SC = 13

2:Aishi Manula – Simba SC = 10.

3:Ali Ahmada – Azam FC = 8.

4:Said Kipao – Kagera Sugar FC = 6.

5:Metacha Mnata – Singida Big Stars = 6.

6:Mohmoud Mroivili – Coastal Union = 6.

7:David Kissu – KMC FC = 5.

8:Jonathan Nahimana – Namungo FC = 5

9:Hussein Abell – Tanzania Prisons = 4.

10:Aaron Kalambo – Dodoma Jiji FC = 4.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live