Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ligi ya Uturuki yasitishwa baada ya rais wa klabu kumpiga ngumi refa

Ligi Ya Uturuki Yasitishwa Baada Ya Rais Wa Klabu Kumpiga Ngumi Refa Ligi ya Uturuki yasitishwa baada ya rais wa klabu kumpiga ngumi refa

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: Bbc

Viongozi wa mchezo wa kandanda nchini Uturuki wamesimamisha ligi zote baada ya refa kupigwa ngumi na rais wa klabu kufuatia mchezo wa ligi kuu siku ya Jumatatu.

Halil Umut Meler alipigwa na rais wa MKE Ankaragucu, Faruk Koca, ambaye alikimbia uwanjani baada ya timu yake kufungwa bao la kusawazisha dakika ya 97 katika sare ya 1-1 ya Super Lig na Caykur Rizespor.

"Mechi katika ligi zote zimeahirishwa kwa muda usiojulikana," mwenyekiti wa FA [TFF] wa Uturuki Mehmet Buyukeksi alisema katika mkutano na waandishi wa habari.

"Shambulio hili ni aibu kwa soka la Uturuki," aliongeza.

Meler alipokea vipigo kadhaa kutoka kwa wengine alipokuwa amelala kwenye nyasi na kupata majeraha ikiwa ni pamoja na kuvunjika kidogo.

Tukio hilo lilizua taharuki iliyohusisha wachezaji na viongozi wa klabu.

Koca alihitaji matibabu hospitalini lakini "taratibu za kuwekwa kizuizini zitatekelezwa baada ya matibabu," alisema waziri wa mambo ya ndani wa Uturuki, Ali Yerlikaya.

Yerlikaya aliongeza wengine wamekamatwa kwa mchango wao katika tukio hilo, ambalo "alililaani vikali".

Baada yya matukio hayo ya kushangaza Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alisema: "Ninalaani shambulizi dhidi ya refa Halil Umut Meler baada ya mechi ya MKE Ankaragucu-Çaykur Rizespor iliyochezwa jioni ya leo, na ninamtakia ahueni ya haraka," alisema.

"Michezo ina maana ya amani na udugu. Michezo haiendani na vurugu. Hatutaruhusu vurugu kutokea katika michezo ya Uturuki."

Klabu ya MKE Ankaragucu ilijutia hatua ya rais wao, ikisema katika taarifa yake: "Tunasikitishwa na kitendo kilichotokea jioni ya leo.

Chanzo: Bbc