Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ligi ya Mabingwa makundi hatma ni leo

Uefa Pic Data Lionel Messi

Wed, 8 Dec 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Leo ndio leo. Hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya inatarajiwa kukamilishwa leo ambapo viwanja mbali mbali barani Ulaya vitawaka moto.

Pale Allianz Stadium Jijini Turin, wababe Juventus watakuwa na kibarua mbele ya Malmo saa 2:45 usiku katika mechi ambayo Malmo atakuwa hana cha kupoteza kwa sababu imeshatolewa lakini Juventus itahitaji kushinda na kuiombe mabaya Chelsea ili kuongoza kundi H.

Chelsea na Juventus zote zina alama 12 hivyo mmoja kati yao akipoteza atampa nafasi mwenzake ya kuongoza kundi lakini zote zikishinda Chelsea itaongoza kwa sababu ya rekodi zake ilipokutana na Juve kwenye hatua hii.

Chelsea itakuwa ugenini kucheza dhidi ya Zenit St. PetersburgĀ  saa 2:45 usiku. Kimbembe kitakuwa pale kundi H ambalo hadi sasa hakuna mwenye uhakika wa kupanda wala kushuka.

VfL Wolfsburg yenye alama tano na kushika mkia kwenye kundi itacheza dhidi ya LOSC Lille inayoongoza kundi kwa alama nane. Ikiwa Wolfsburg itashinda kuna uwezekano mkubwa ikafuzu hatua ya 16 bora au mtoano Europa kwa kuangalia matokeo kati ya timu zinazoshika nafasi yapili na ya tatu ambapo RB Salzburg itakuwa inacheza dhidi ya Sevilla saa 5:00 usiku.

Sevilla ina alama tano na Salzburg pia ina ala tano. Hivyo timu zote zina nafasi ya kufuzu Mtoano Uefa au Europa kwa kuangalia matokeo ya mwisho.

Bayern Munich ambayo inaongoza kundi E itakuwa inacheza bila ya presha dhidi ya Barcelona kwa sababu imeshafuzu lakini Barcelona itahitaji kushinda mechi hiyo ili kufuzu hatua inayofuata na kama haitofanya hivyo itaangukia Europa ikiwa Benfica itashinda mechi yao dhidi Dynamo Kiev kwa sababu Barca ina alama saba na Benfica ina alama tano.

Wakati Man United ikiwa haina presha baada ya kujihakikishia nafasi ya kufuzu hatua ya 16 bora. kazi ngumu itakuwa kati ya Atalanta ambazo mmoja wao Villarreal inatakiwa kushinda ili kusonga mbele huku Atalanta itatakiwa kutoa sare ili kusonga.

Lakini Villarreal ikitoa sare na Young Boys ikashinda mbele ya Man United Villa itakosa nafasi hata yakufuzu hatua ya mtoano ya michuano ya Europa. Mechi zote hizi zitapigwa saa 5:00 usiku.

Matokeo ya jana

FC Porto 1-3 Atletico Madrid Shakhtar Donetsk 1-1 Sheriff Tiraspol Dortmund 5-0 Besiktas AC MilanĀ  1-2 Liverpool Real Madrid 2-0 Inter Millan AFC Ajax 4-2 Sporting CP RB Leipzig 2-1 Manchester City PSG 4-1 Club Brugge

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz