Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ligi inarejea, rekodi za Wananchi Ligi Kuu zinatisha

Tano Ta Yanga Rekodi za Wananchi Ligi Kuu zinatisha

Sun, 28 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa imesimama na kutarajiwa kurejea hivi karibuni, timu ya Young Africans SC imekuwa na rekodi bora msimu huu wa 2023-2024.

Young Africans SC ambayo imeshuka dimbani mara 11 na kukusanya pointi 30, huku ikishika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo, ina rekodi kadhaa za kuvutia.

Miongoni mwa rekodi hizo ni timu pekee ambayo haijapata sare katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu mpaka sasa, huku ikiwa ndiyo imeruhusu magoli machache zaidi yakiwa ni sita. Katika mechi hizo 11, Young Africans SC imeshinda mechi 10 na kupoteza moja, huku ikifunga magoli 31.

Ukiachana na hilo, kubwa zaidi ni kwamba, Young Africans SC ndiyo timu pekee katika mechi zake zote za Ligi Kuu Tanzania msimu huu wa 2023/2024, imeanza kufunga goli, haijawahi kutanguliwa na mpinzani. Hata katika mchezo huo mmoja ambao tumepoteza, tulianza kufunga goli, wapinzani wakafuatia.

Katika magoli 31 yaliyofungwa na Young Africans SC, kipindi cha pili yamepatikana mengi zaidi ambayo ni 20, huku kipindi cha kwanza yakifungwa magoli 11.

Stephane Aziz Ki, ndiye mchezaji aliyefunga magoli mengi katika mechi tofauti kushinda wachezaji wengine wa Young Africans SC akifanikiwa kufunga katika mechi saba kati ya 11 ambazo timu imecheza.

Katika mechi hizo saba alizofunga Aziz Ki, ameweka kambani magoli kumi na kuwa kinara ndani ya kikosi cha Young Africans SC, sambamba na Ligi Kuu kwa jumla.

Ndani ya Yanga, anafuatiwa na Maxi Nzengeli ambaye amefunga magoli saba katika mechi nne tofauti, wakati Pacome Zouzoua naye akifunga magoli manne katika mechi nne tofauti.

MATOKEO YA MECHI HIZO YAPO HIVI;

AGOSTI 23, 2023

Yanga 5-0 KMC

WAFUNGAJI YANGA:

Dickson Job (DK 17)

Aziz Ki (DK 58)

Hafiz Konkoni (DK 69)

Mudathir Yahya (DK 76)

Pacome Zouzoua (DK 81)

AGOSTI 29, 2023

Yanga 5-0 JKT Tanzania

WAFUNGAJI YANGA:

Aziz Ki (DK 45+5)

Kenendy Musonda (DK 54)

Yao Attohoula (DK 64)

Maxi Nzengeli (DK 79)

Maxi Nzengeli (DK 87)

SEPTEMBA 20, 2023

Yanga 1-0 Namungo

MFUNGAJI YANGA:

Mudathir Yahya (DK 88)

OKTOBA 4, 2023

Ihefu 2-1 Yanga

MFUNGAJI YANGA:

Pacome Zouzoua (DK 3)

WAFUNGAJI IHEFU:

Lenny Kissu (DK 40)

Charles Ilanfya (DK 67)

OKTOBA 7, 2023

Geita 0-3 Yanga

WAFUNGAJI YANGA:

Pacome Zouzoua (DK 44)

Aziz Ki (DK 45+2)

Maxi Nzengeli (DK 69)

OKTOBA 23, 2023

Yanga 3-2 Azam

WAFUNGAJI YANGA:

Aziz Ki (DK 8)

Aziz Ki (DK 64)

Aziz Ki (DK 71)

WAFUNGAJI AZAM:

Gibril Sillah (DK 18)

Prince Dube (DK 62)

OKTOBA 27, 2023

Yanga 2-0 Singida Fountain Gate

WAFUNGAJI YANGA:

Maxi Nzengeli (DK 30)

Maxi Nzengeli (DK 39)

NOVEMBA 5, 2023

Simba 1-5 Yanga

WAFUNGAJI YANGA:

Kennedy Musonda (DK 3)

Maxi Nzengeli (DK 64)

Aziz Ki (DK 73)

Maxi Nzengeli (DK 77)

Pacome Zouzoua (DK 87 penalti)

MFUNGAJI SIMBA:

Kibu Denis (DK 9)

NOVEMBA 8, 2023

Coastal 0-1 Yanga

MFUNGAJI YANGA:

Clement Mzize (DK 71)

DESEMBA 16, 2023

Yanga 4-1 Mtibwa

WAFUNGAJI YANGA:

Aziz Ki (DK 45 penalti)

Aziz Ki (DK 65)

Kennedy Musonda (DK 76)

Skudu Makudubela (DK 83)

MFUNGAJI MTIBWA:

Seif Karihe (DK 90+5)

DESEMBA 23, 2023

Tabora United 0-1 Yanga

MFUNGAJI YANGA:

Aziz Ki (DK 21)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live