Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ligi imeisha, Simba nafasi ya pili ni ngumu - Mchambuzi

Saido Mknb Ligi imeisha, Simba nafasi ya pili ni ngumu - Mchambuzi

Wed, 22 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka Clouds Media, Master Tindwa amesema kwa mwenendo ulivyo ni kama Ligi imeisha na uwezekano wa Simba kumaliza nafasi ya pili.

Simba ambaye analingana na Azam kwa alama 63 kila mmoja lakini Azam yupo juu kwenye msimamo wa ligi kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa huku kila mmoja akipigania nafasi ya pili ili aweze kushiriki Klabu Bingwa Afrika msimu ujao.

“Kama Azam atafunga goli moja kila mechi kwa mechi zilizobaki, Simba inabidi wafunge magoli manne kila mechi ili wamalize nafasi ya pili, inawezekana lakini sio rahisi.

“Naona nafasi ya pili kwa Simba ni ngumu , Ligi tayari imeisha wa mwisho watakuwa walivyo na juu itabaki ilivyo ,Kila mtu anaomba ashinde mechi zake na mwisho wa siku Azam tayari anafaida,” amesema Tindwa.

Mechi za Simba zilizobaki

Vs KMC

Vs JKT Tanzania

Mechi za Azam zilizobaki

Vs Kagera

Vs Geita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live