Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ligi Kuu kuendelea leo

Geita Vs Prisons.jpeg Ligi Kuu kuendelea leo

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea leo Jumatano, Novemba 22, 2023 kwa michezo miwili kufanyika Geita na Kagera.

Geita Gold inayoshika nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 7 baada ya michezo 9 itakuwa mwenyeji wa JKT Tanzania iliyopo nafasi ya sita ikiwa na pointi 14 kwenye uwanja wa Nyankumbu, Geita.

KMC yenye pointi 15 katika nafasi ya tano itakuwa mgeni wa Kagera Sugar inayoshika nafasi ya nane ikikusanya pointi 12 katika msimamo wa ligi kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live