Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ligi Kuu imesimama Timu zijipange

Yanga X Simba Balaa Ligi Kuu imesimama Timu zijipange

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Ligi Kuu inasimama kwa muda kupisha kalenda ya michuano ya kimataifa na itarejea tena Oktoba 23. Ni takribani wiki mbili mashabiki wa soka nchini watakosa uhondo wa ligi hiyo ambayo inazidi kushika kasi kwa miamba ya soka nchini kutambiana na jana kulipigwa michezo miwili na Singida Fountain Gate iliikaribisha Simba huku Tanzania Prisons iliikaribisha Mtibwa Sugar.

Michezo hiyo miwili inakaribisha kipindi hicho cha wiki mbili kupisha kalenda hiyo ya kimataifa.

Hakuna namna linapokuja suala la kalenda ya kimataifa ya Shirikisho la Soka Duniani na ni kipindi hicho timu za Taifa zinakuwa kwenye michuano husika ingawa kwa sasa Tanzania haina mchezo wowote lakini ni lazima ipishe kalenda hiyo ya kimataifa.

Hata hivyo, mara nyingi linapokuja suala kama hili la kalenda ya FIFA, kumekuwa na kupooza kwa amshaamsha ya Ligi Kuu na mashabiki hulazimika kusubiri hadi itakaporejea ndipo waendelee na uhondo huo.

Ratiba ya msimu huu mechi zake zimekuwa zikichezwa na kupumzika kwa muda mrefu jambo ambalo mashabiki wengi wamekuwa wakilalamikia na kuona timu zinakaa muda mrefu bila ya kucheza.

Sisi kama wadau wa kubwa wa soka tunaamini ni kweli kalenda ya Fifa ni muhimu kufuatwa lakini pia ratiba ingepangwa vizuri ili kuifanya michezo mingine baadhi ichezwe na sio kusimama kwa muda mrefu.

Hata hivyo hilo liko chini ya Bodi ya Ligi na kilichopo kwa sasa ni kwa timu shiriki za ligi hiyo kuendelea na maandalizi yao zikisubiri ligi irejee.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: