Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ligi Kuu bora Ulaya nusu fainali Qatar

Ligi Bora Ulaya Pic Ligi Kuu bora Ulaya nusu fainali Qatar

Thu, 15 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Vigogo wanne, Argentina, Croatia, Ufaransa na Morocco ndiyo waliotinga nusu fainali ya fainali za Kombe la Dunia 2022 huko Qatar, ambapo fainali yake itapigwa Jumapili.

Argentina juzi Jumanne ilikata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuwachapa Croatia 3-0 na usiku wa jana Jumatano kulikuwa na kipute kingine kilichozikutanisha Morocco na Ufaransa. Mshindi atakwenda kucheza fainali, wakati aliyechapwa atakipiga na Croatia kwenye mchezo wa kusaka tatu bora.

Wakati fainali hizo zinaingia kwenye nne bora, kuna Ligi Kuu tano bora za Ulaya ndizo zilizoongoza kuwa na wachezaji wengi ambao wamezisaidia timu zao kufika hatua hiyo. Ligi hizo zilizoongoza kwa kuwa na wachezaji wengi kwenye hatua ya nusu fainali kwenye Kombe la Dunia 2022 huko Qatar ni hizi hapa.

5. Bundesliga (wachezaji 13)

Klabu iliyokuwa na wachezaji wengi kutoka Bundesliga katika hatua hiyo ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2022 huko Qatar ni Bayern Munich, ambayo ilikuwa na mastaa sita. Kwa ujumla wake, Bundesliga iliingiza wachezaji 13.

Bayern Munich ni Josip Stanisic, Kingsley Coman, Lucas Hernandez, Benjamin Pavard, Dayot Upamecano na Noussair Mazraoui.

Stuttgart ni Borna Sosa

Hoffenheim ni Andrej Kramaric

Eintracht Frankfurt ni Kristijan Jakic, Randal Kolo Muani.

Borussia Monchengladbach ni Marcus Thuram.

Bayern Leverkusen ni Exequiel Palacios

4. Serie A (wachezaji 14)

Serie A imekuwa na klabu nyingi zilizotoa wachezaji kushiriki kwenye fainali za Kombe la Dunia 2022 na kutinga hatua ya nusu fainali. Kuna wachezaji 10 kutoka timu 10 tofauti za Serie A ambazo mastaa wake wametinga nne bora Qatar.

Inter Milan ni Lautaro Martinez, Marcelo Brozovic

Juventus ni Leandro Paredes, Angel Di Maria, Adrien Rabiot

AS Roma ni Paulo Dybala

Sassuolo ni Martin Erlic

Atlanta ni Mario Pasalic

Tornio ni Nikola Vlasic

AC Milan ni Theo Hernandez, Oliver Giroud

Fiorentina ni Sofyan Amrabat

Sampdpria ni Abdelhamid Sabiri

3. Ligue 1 (wachezaji 14)

Ligi Kuu Ufaransa (Ligue 1) nayo imekuwa na idadi kubwa ya mastaa waliotinga nusu fainali kwenye Kombe la Dunia. Lionel Messi, Kylian Mbappe na Achraf Hakimi wao wanatoka kwenye kikosi cha PSG, huku kukiwa na klabu nyingine kadhaa kutoka kwenye ligi hizo zikiwa na mastaa wengi nusu fainali.

PSG ni Lionel Messi, Kylian Mbappe, Achraf Hakimi

Lyon ni Nicolas Tagliafico

Rennes ni Lovro Majer, Steve Mandanda

Monaco ni Axel Disasi Youssouf Fofana, Jordan Veretout.

Marseille ni Matteo Guendouzi

Brest ni Achraf Banoun

Toulouse ni Zakaria Aboukhlal

2. Premier League (wachezaji 16)

Kuna timu sita kutoka kwenye Ligi Kuu England zilizoingiza mastaa wengi kwenye nusu fainali ya Kombe la Dunia huko Qatar. Tottenham Hotspur, Manchester United, Aston Villa, Chelsea, West Ham United, Liverpool, Arsenal, Brighton, na Manchester City zote zimeingiza wachezaji kwenye hatua hiyo, huku jumla yake wakiwa 16.

Aston Villa ni Emiliano Martinez

Tottenham ni Ivan Perisic, Hugo Lloris, Cristian Romero

Man United ni Raphael Varane, Lisandro Martinez

Man City ni Julian Alvarez

Chelsea ni Mateo Kovacic

Arsenal ni William Saliba

Liverpool ni Ibrahima Konate

West Ham ni Nayef Aguerd, Alphonse Areola

Brighton ni Alexis Mac Allister

1. La Liga (wachezaji 22)

Ligi nyingine kubwa iliyoingiza wachezaji wengi kwenye nne bora ya fainali za Kombe la Dunia 2022 huko Qatar ni La Liga. Kuna wachezaji 22 wa kutoka ligi hiyo waliingia kwenye nusu fainali ya Kombe la Dunia huko Qatar, huku Atletico Madrid ikiingiza mastaa watano kwenye hatua hiyo na La Liga ikiwa na timu nane tofauti zenye mastaa wake nusu fainali Qatar.

Barcelona ni Ousmane Dembele, Jules Kounde

Real Madrid ni Aurelien Tchouameni, Luka Modric and Eduardo Camavinga

Atletico Madrid ni Nahuel Molina, Rodrigo de Paul, Angel Correa, Ivo Grbic, Antoine Griezmann.

Villarreal ni Geronimo Rulli and Juan Foyth

Sevilla ni Gonzalo Montiel, Acuna, Alejandro Gomez, Yassine Bounou, Youssef En-Nesyri.

Real Betis ni German Pezzella, Guido Rodriguez

Osasuna ni Ante Budimir, Ez Abde.

Real Valladolid ni Jawad El Yamiq

Chanzo: Mwanaspoti