Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ligi Kuu Wanawake kuendelea Leo Viwanja mbalimbali.

Ligi Wanawake Logo Ligi ya wanawake kuendelea Leo

Sun, 26 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ligi Kuu ya soka ya wanawake Tanzania ya Serengeti Lite inaendelea leo kwa michezo minne kwenye viwanja tofauti nchini.

JKT Queens itakuwa uwanja wa nyumbani wa Mej Gen Isamuhyo, Dar es Slaam kuikaribisha Oysterbay Girls wakati The Tigers Queens itakuwa wageni wa TSC Queens kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Nao Ilala Queens watakuwa wageni wa Fountain Gate Princess kwenye uwanja wa Fountain Gate huku Baobao Queens wakiwakaribisha Yanga Princess kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Katika michezo miwili ya ufunguzi ya ligi hiyo iliyopigwa Desemba 23 Simba Queens imeichapa bila huruma Ruvuma Queens kwa mabao 15-0 kwenye uwanja wa Mo Simba Arena, Dar es Salaam wakati Alliance Girls imeifunga Mlandizi Queens kwa bao 1-0 kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live