Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Licha ya kichapo, Kocha Canada awapongeza wachezaji

Canada Lost Licha ya kichapo, Kocha Canada awapongeza wachezaji

Thu, 24 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa timu ya Taifa ya Canada John Herdman amesema amefurahishwa na kiwango bora cha timu yake licha ya kupoteza katika mchezo wao wa ufunguzi dhidi ya Ubelgiji hapo jana.

Kocha huyo amesema licha ya kupoteza mchezo wao jana dhidi ya Ubelgiji lakini walifanikiwa kuonesha soka safi ambalo anaamini inaonesha namna ambavyo walistahili kuwepo kwenye michuano hiyo.

Canada baada ya kukaa miaka 36 bila kushiriki michuano ya kombe la Dunia walianza vibaya jana kwa kufungwa bao moja kwa bila na Ubelgiji bao pekee lililofungwa na Mitchy Batshuayi lilitosha kuipa Ubelgiji alama tatu kwenye mchezo huo.

Kocha Herdman bado anaamini pia timu ya taifa ya Ubelgiji ina ubora mkubwa sana hasa kwenye eneo la ulinzi ambayo ilikua inaundwa na Jan Vertoghen, Leander Dendocker, Toby Alderweirld huku pia akimwaga sifa kwa golikipa Thibaut Cortous.

Timu ya Taifa ya Canada ilifanikiwa kupata mkwaju wa penati mapema wakati mchezo huo unaanza baada ya mchezaji wa Ubelgiji Yannick Carrasco kuunawa mpira kwenye eneo la hatari na mwamuzi kuamuru mkwaju wa penati.

Alikua ni Alphonso Davies beki wa klabu ya Bayern Munich ambaye alichukua jukumu la kupiga mkwaju huo ambapo golikipa Courtous akaweza kuuchomoa mkwaju huo na kuiweka Ubelgiji mikono salama na kuweza kuondoka na alama tatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live