Timu ya taifa ya Libya ipo kwenye mchakato wa kumtafuta Kocha mpya baada ya kumalizana na Corentin Martins, maafisa husika wameeleza nia yao ya kumpata kocha wa mzalendo.
Martins (53) alipewa mkataba wa mwaka mmoja alipochukua nafasi ya Javier Clemente mwezi Aprili mwaka jana.
Taarifa zinaeleza kuwa uamuzi wa kumaliza mkataba huo mapema ulitokana na utendaji mbovu katika michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza Ligi za ndani (CHAN).
Akizungumza na BBC Sport Africa, Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka la Libya Abdul Nasser Ahmed amesema kuwa wanakamati wote walikubaliana kuchagua kocha kutokea Libya.