Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lewis Morgan aongezwa Scotland Euro 2024

Skysports Lewis Morgan New York Red Bulls 6574525 Lewis Morgan aongezwa Scotland Euro 2024

Thu, 6 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mshambuliaji wa Klabu ya New York Red Bulls, Lewis Morgan ameitwa kwenye kikosi cha Scotland siku nane kabla ya kuanza kwa Fainali za Mataifa ya Ulaya ‘Euro 2024’.

Scotland itafungua fainali hizo kwa kucheza dhidi ya wenyeji Ujerumani Ijumaa (Juni 14) kwenye Uwanja wa Allianz Arena.

Morgan ameitwa kikosini akifuatana na mshambuliaji kinda wa kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 21 na Klabu ya Bristol City ya England, Tommy Conway.

Kocha Mkuu wa Scotland, Steve Clarke amefanya uamuzi wa kuwaita wawili hao, baada ya mshambuliaji Lyndon Dykes na winga Ben Doak kupata majeraha.

Hatua ya kujumuishwa kwa Morgan mwenye umri wa miaka 27, inakifanya kikosi cha Scotland kufikisha idadi ya wachezaji 28, ambao watachujwa hadi 26, tayari kwa safari ya Ujerumani.

Mbali na mchezo wa ufunguzi wa Kundi A dhidi ya Ujerumani Juni 14, Waskochi watamenyana na Uswisi Juni 19, kisha watamaliza na Hungary Juni 23.

Kesho Ijumaa Scotland itacheza mchezo wake wa mwisho wa kimataifa wa kirafiki dhidi Finland huko Hampden.

Chanzo: Mwanaspoti