Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lewandowski naye anamtaka Messi

Messi X Lewa.jpeg Lionel Messi sambamba na Robert Lewandowski

Mon, 26 Dec 2022 Chanzo: Mwanasppti

Nyota wa Barcelona, Robert Lewandowski amekiri anatamani kucheza na Lionel Messi lakini itakuwa ngumu staa huyo kurejea ndani ya viunga vya Nou Camp kwasasa.

Licha ya kauli ya Lewandowski staa huyo anayekipiga Paris-Saint Germain yupo mbioni kusaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki Parc des Princes.

Lewandowski ambaye kwasasa ndiye anayeingoza Barcelona, amesema anavutiwa na uchezaji wa Messi aliyebeba Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza.

“Sio mimi tu, wapo wachezaji wengine wenye ndoto ya kucheza na Messi kabla hajastaafu soka, tofauti na miaka iliyopita kila mtu anatamani sana, amepata mafanikio makubwa kwenye fainali za Kombe la Dunia Qatar,” alisema Lewandowski.

Alipoulizwa kama Messi ana nafasi nzuri ya kubeba tuzo ya nane ya Ballon d’Or, Lewandowski akajibu: “Messi amefanya mambo makubwa Qatar, nandhani ana nafasi nzuri, kwasasa anafurahia mafanikio yake aliyopata.”

Lewandowski aliiongoza Poland kwenye fainali za Kombe la Dunia zilizomalizika Qatar hata hivyo ikashindwa kutoboa na ikatolewa raundi ya 16 bora dhidi ya Ufaransa kwa mabao 3-1.

Lewandowski alipata mafanikikio kipindi alipokuwa akikipiga Bayern Munich kabla ya kuondoka katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi nafasi yake ikizibwa na Sadio Mane kutoka Liverpool.

Chanzo: Mwanasppti