Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lewandowski azidi kuweka alama Bundasliga, avunja rekodi ya miaka 49

Lewa Goals Robert Lewandowski

Sat, 18 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bayern Munich imeichapa bao 4-0 Wolfsburg ambapo mshambuliaji wa kati wa timu hiyo Robert Lewandowski ametupia bao moja na kuipa uhakika wa ushindi Munich ambao wanalikimbiza taji la Bundesliga.

Mabao ya Munich yamefungwa na Thomas Muller(ambaye ilikuwa mechi ya 400), Leroy Sane na Dayot Upamecano ambapo sasa wanaendelea kuwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Ujerumani kwa tofauti ya alama tisa dhidi ya timu iliyo nafasi ya pili Borussia Dortmund.

Bao la Lewandowski ni goli la 43 la msimu huu kwa Bayern Munich akiipiku rasmi rekodi ya mkali mwingine wa mabao Gerd Muller ambayo imedumu tangia mwaka 1972.

Matokeo hayo yanaifanya Wolfsburg kusalia nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Bundesliga na Munich kileleni mwa msimamo huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live