Robert Lewadowski amechukizwa na kitendo cha Bayern Munich kumpoteza na mawazo yao yote wakiweka kwa Erling Haaland aliyekubali kujiunga na Manchester City kwa kitita cha Pauni 51 mbioni.
Bayern imemfukuzia Haaland kwa muda mrefu kama mbadala wa Lewandowski endapo ataondoka klabuni humo.
Kwa sasa Lewandowski amebakiza mkataba wa mwaka mmoja ambao utaisha itakapofika mwaka 2023, lakini hakuna mazungumzo ya kujadili kuhusu uwezekano wa straika huyo kusaini mkataba mwingine.
Kwa mujibu wa gazeti la Mundo Deportivo limeripoti Lewandowski anahisi Bayern Munich imekosea heshima licha ya mchango wake Allianz Arena kwa muda wa miaka minane aliyokuwa akikipiga humo.
Imeelezwa Bayern ilikuwa ikimfukuzia Haaland tangu wikiendi iliyopita lakini Manchester City ikafanikiwa kunasa saini ya kali huyo wa mabao wa Borrusia Dortmund.
Hata hivyo, Bayern inaamini Lewandowski atabaki na wana mpango wa kupiga chini ofa yoyote itakayotolewa na klabu ambayo inahitaji huduma yake.
Taarifa zimezidi kuchimba mastaa wengi hawakufurahishwa na kitendo cha timu wanazocheza kumtolea macho straika huyo wa Kimataifa wa Norway.
Mbali na Lewandowski, Ousmane Dembele alichukizwa pia na kitendo cha Barcelona kumpotezea huku tetesi zikiripoti Haaland anatolewa macho na miamba hiyo ya La Liga.
Hata hivyo, Barcelona imepata ahueni na kumpotezea Haaland tangu Pierre-Emerick Aubameyang alipojiunga akitokea Arsenal dirisha dogo la usajili Januari, mwaka huu kutokana na mchango wake.