Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lewandowski awapa tahadhari Bayern Munich

Lewandowski Goals Roberto Lewandowski

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa Barcelona, Robert Lewandowski amewapa tahadhari timu yake ya zamani Bayern Munich kwamba Real Madrid ni sio timu ya kuichukulia poa, ameyasema hayo alipozungumza na mtandao wa Sport BILD kuelekea mchezo wa Nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya ambapo Bayern Munich atamenyana na Real Madrid

"Huwezi kamwe kuwadharau Real Madrid. Wanashinda mechi ambazo huwezi kuamini, huwezi kuelezea. Real Madrid hawafi kamwe. Hawakati tamaa. Wanacheza kama timu uwanja mzima. Wakati mwingine unaweza kudhani unakaribia kushinda, lakini mwishowe hushindi".

"Hata hivyo Bayern wana nafasi, lazima wafanye vizuri katika mechi hii ya nyumbani, mechi ya Bernabeu ni tofauti mambo mengi ya nje ya Uwanja yanaweza kuamua mchezo hili nimelijua hivi punde. Natamani Bayern waifunge Real Madrid, nawaombea" amesema Lewandowski

Chanzo: www.tanzaniaweb.live