Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lewandowski ajitetea ishu ya Lamine

Fc Barcelona Unveil New Signing Robert Lewandowski Scaled 1 1024x683 Lewandowski ajitetea ishu ya Lamine

Thu, 16 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kushutumiwa kwa kumpuuza mchezaji mwenzake wa Barcelona, Lamine Yamal wakati wa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Alaves, Robert Lewandowski amejibu.

Fowadi huyo alikuwa gumzo la jiji wikiendi iliyopita huko Barcelona baada ya mabao yake mawili kuisaidia timu kuibuka na ushindi huo.

Lakini, mashabiki wa klabu hiyo hawakuridhika na straika huyo ambaye picha zake zinamwonyesha akimpuuza kinda wa Yamal wa wakati wa mechi hiyo.

Wakati wa mechi Lewandowski alionekana kama anamfokea kinda huyo mwenye umri wa 16, cha kushangaza baada ya mechi Lamine alipeana mikono na wachezaji wenzake lakini akampotezea straika huyo wa zamani wa Bayern Munich.

Kitendo hicho cha Lewandowski kiliwashangaza mashabiki kwani imeashiria hana mapenzi na kinda huyo mwenye kipaji kikubwa cha soka.

Akizungumzia hilo wakati anajiunga na timu ya taifa ya Poland, Lewandowskialisema; “Kumpuuza Lamine Yamal? Hakuna chochote cha kuzungumzia, ilikuwa bahati mbaya tu. Wakati mwingine mimi napenda kupiga kelele wakati wa mechi, lakini hiyo ni kawaida.”

Aidha kocha Xavi Hernandez amezungumza sana kuhusu mazingira yanayowahusu wachezaji wake kwenye vyumba vya ku-badilishia nguo na mara kwa mara alimpongeza mshambuliaji wake, kwani ni mfano kwa wachezaji wenye umri mdogo kama Lamine, Pedri na Gavi.

Kabla ya kurejea Barcelona kuwavaa Rayo Vallecano kwenye mechi ya La Liga, mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Poland atakuwa bize na majukumu ya kitaifa dhidi ya Czechia na Latvia kwenye mechi ya kufuzu Euro 2024.

Lewandowski alifunga mabao mawili moja la mkwaju wa penalti kwa mara kwanza dhidi ya Alaves tangu alipofunga mabao mawili dhidi ya Celta Vigo Septemba 23.

Chanzo: Mwanaspoti