Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lewandowski aendelea kutema nyongo Bayern

Lewaaa Mshambuliaji wa Bayern Munchen Robert Lewandowski

Tue, 7 Jun 2022 Chanzo: eatv.tv

Nyota wa Bayern Munich, Robert Lewandowski ameendelea kuisakama klabu hiyo kwa mara nyingine tena akisema kwamba kuna kitu 'kimekufa' ndani yake kwa wababe hao wa Ujerumani na kwa kumweka hapo kinyume na matakwa yake kutaharibu tu sifa yao huko mbeleni.

Lewandowski amekuwa akiongea hadharani kuhusu nia yake ya kutaka kuihama Bayern Munchen majira haya ya joto, na kwasasa anaweka nguvu ya ushawishi kwa timu hiyo kufikiria kumuuza huku klabu ya Barcelona ikiwa ni mahali pekee anapo pendelea zaidi kucheza msimu ujao.

Mwezi uliopita mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 aliwasilisha ombi la kutaka kuhama na pia hakusita kuishutumu timu yake ya sasa kwa kukosa uaminifu na heshima baada ya miaka minane aliyo hudumu na kuwawezesha kubeba mataji.

Chanzo: eatv.tv