Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Leverkusen wana jambo lao msimu huu

Roma Leverkusen Sportstiger 1683636843987 Original Leverkusen wana jambo lao msimu huu

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Bayern Leverkusen, Xabi Alonso ambaye timu yake pamoja na Bayern Munich zikiwa ndizo timu mbili pekee ambazo hazijaonja kushindwa msimu huu katika Bundesliga anasema, kibarua bado ni kikubwa kwa vijana wake licha ya matokeo mazuri wanayoendelea kuyapata kuelekea mapumziko ya Krismasi na majira ya baridi ya Bundesliga.

"Kwa kweli tutahitajika kujituma mno kwasababu tuna mechi nyingi katika wiki chache tu, ila tunajua kinachohitajika na bila shaka tutakuwa tayari. Wacha tu tuone jinsi mambo yatakavyokwenda," alisema Alonso.

Naye mchezaji wa kiungo cha kati wa Leverkusen Florian Wirtz ambaye amekuwa mmoja wa nyota wa timu hiyo msimu huu, hapa anaeleza kilichowapelekea kupata ushindi wa mabao matatu ugenini dhidi ya Bremen.

"Ingawa tulikwenda mapumzikoni tukiwa na uongozi wa 2-0, sifikiri kama tuliridhika na mambo yalivyokuwa. Tuliendelea kupambania malengo yetu na kazi tukaifanya mpaka mwisho," alisema Wirtz.

Baada ya mechi 12 Leverkusen sasa wanaliongoza jedwali la Bundesliga wakiwa na pointi 34 na wanaowafuata ni Bayern Munich walio na jumla ya pointi 32.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live