Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Leopards yachapwa 4-1 na Bidco FC

Leopards Vs Bico United.jpeg Leopards yachapwa 4-1 na Bidco FC

Mon, 9 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha AFC Leopards kimekutana na kipigo kizito kutoka kwa Bidco United cha bao 4-1 huku kocha wa Ingwe Patrick Aussems akidai kuwa makosa ya kiulinzi yamepelekea kukutana na kichapo hicho.

Kikiwa ni kipigo kikubwa kukipata baada ya muda mrefu, AFC Leopards wanajiandaa kuwa vizuri kwa mchezo ujao ambapo Aussems ameandika kwenye kurasa zake za kijamii kuwa “tunashinda pamoja na kupoteza pamoja”.

Kwa matokeo hayo, AFC Leopards wanashika nafasi ya 11 wakiwa na alama nane baada ya kucheza mechi saba wakati Bidco wakikwea mpaka nafasi ya 12 alama saba na michezo saba.

Mechi ijayo kwa AFC Leopards itakuwa dhidi ya kibonde Wazito FC ambaye hajashinda mchezo wowote mpaka sasa siku ya Jumamosi.

Baadhi ya mechi ambazo zimechezwa wikiendi hiyo ni pamoja na Bandari 2-1 Tusker, Posta Rangers 0-2 Gor Mahia, Vihiga Bullets 4-2 Nairobi City Stars na Mathare United 0-4 Sofapaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live