Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Leonel Ateba arithishwa mikoba ya Mayele Young Africans

F XbUA8W0AAEajn Leonel Ateba arithishwa mikoba ya Mayele Young Africans

Thu, 28 Dec 2023 Chanzo: Dar24

Uongozi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans umekamilisha dili na kuinasa saini ya Mshanmbuliaji kutoka Klabu ya Dynamo Dougla ya Cameroon, Leonel Ateba, kwa mkataba wa miaka miwili.

Young Africans imemsajili mshambuliaji huyo kwa mapendekezo ya Kocha wao Miguel Gamondi aliyetaka kusajiliwa mshambuliaji mwingine mwenye uwezo wa kufunga.

Taarifa zinaeleza kuwa, Mshambuliaji huyo atakuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo inayokwenda visiwani Zanzibar katika michuano ya Kombe la Mapinduzi na kuanza mechi ya kwanza dhidi ya Jamhuri, Desemba 31, mwaka huu.

Imefahamika kuwa tayari mshambuliaji huyo amemalizana na Young kwa ajili ya kuja kuziba nafasi ya Fiston Mayele ambayo hadi sasa walikuwa hawajapata mrithi wake na wanaamini anakuja kukata kiu yao.

“Ateba amemalizana na Young Africans na muda wowote anatua nchini kuungana na kikosi kwa ajili ya kwenda visiwani Zanzibar kwenye michezo ya Kombe la Mapinduzi, atakuwa sehemu ya kikosi na amesaini mkataba wa miaka miwili,” amesema mtoa habari huyo.

Ameongeza kuwa ujio wa mshambuliaji huyo unawafungulia mlango wa kutokea nyota wawili, Hafiz Konkoni na Gift Freddy ambao watatolewa kwa mkopo baada ya kushindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza na kushindwa kumshawishi Kocha Gamondi kuwapa namba.

Alipotafutwa Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema usajili umeshafanyika na wamekamilisha kila kitu, huku wachezaji wao wapya wakitarajiwa kuonekana katika Kombe la Mapinduzi.

“Tumefanya usajili kulingana na mahitaji ya benchi la ufundi, moja ya sajili zetu tutaziona katika mechi zetu za Mapinduzi tukianza dhidi ya Jamhuri,” amesema Kamwe.

Ameongeza kuwa kikosi cha timu hiyo kinatarajia kuondoka leo Ahamis (Desemba 28) kuelekea visiwani Zanzibar, huku wakitangaza hali ya hatari kwa wapinzani wao kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Young Africans wanaondoka na wachezaji wote ambao hawako katika majukumu ya timu zao za Taifa, pamoja na wachezaji wapya ambao wamesajiliwa kipindi cha dirisha dogo ambalo linatarajiwa kufungwa Januari 15, 2024.

Chanzo: Dar24
Related Articles: