Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Leonardo: Tupo kwenye nafasi nzuri ya kumbakisha Mbappe

Mbappe Le Mbappe anawindwa kwa karibu na Real Madrid

Mon, 20 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya PSG Leonardo amesisitiza kuwa wapo kwenye nafasi nzuri ya kuhahakikisha kuwa mshambuliaji wao hatari Kylian Mbappe anabaki klabuni licha ya kuwa mkataba wake unaisha majira ya kiangazi.

Mbappe mwenye umri wa miaka 22 ameifungia klabu hiyo magoli 145 kwenye michezo 194 katika mashindano yote tokea aliposajiriwa mwaka 2018 akitokea klabu ya Monaco na kwenye usajiri uliomfanya kuwa mchezaji ghali wa pili duniani wa muda wote.

“Ni swala muhimu sababu tunazungumzia mchezaji bora wa Dunia ambaye mkataba wake unakwenda kuisha, tunaweza kusema tumezungumza nae mara nyingi kwa njia ya kinyenyekevu zaidi, lakini ndio sehemu ya kujenga mahusiano.

“Kuna gumu kidogo ila kwa namna nyingine tungependa aendelee kuwepo maisha yake yote hapa na pia itatupasa kuheshimu nafasi ya familia yake, nadhani tunanafasi nzuri ya kuhakikisha anasalia hapa, naamini hilo.” Alisema Leonardo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live