Beki wa kimataifa wa Italia na Klabu ya Juventus Leonardo Bonucci, amesema anatarajia kustaafu mwishoni mwa msimu ujao mkataba wake ndani ya klabu hiyo utakapofikia mwisho.
Bonucci ambaye amekua kwenye klabu ya Juventus kwa muda mrefu akiitumikia timu hiyo na kushinda mataji mengi ametangaza kustaafu baada ya msimu ujao kum alizika atatundika daluga akiwa na umri wa miaka 37.
Beki huyo amesema hayo alipohojiwa na Mtandao wa You Tube wa klabu hiyo na kuongeza anakwenda kustaafu mwakani itakua ndio mwisho wa zama za uzuiaji kwa staili ya kiitaliano kama ambavyo walikua wakifanya wao na waliopita huko nyuma.
Bonucci ambaye ameitumikia Juventus michezo 500 mpaka sasa ameibua maswali kutokana na kauli yake hiyo ya kusema akistaafu yeye ndio utakua mwisho wa uzuiaji wa aina ya kiitaliano.
Hii imeonyesha beki huyo haoni beki mwingine wa Kiitaliano ambaye atafuata nyendo zao.
Bonucci atakumbukwa kwa mafanikio makubwa aliyoyapata ndani ya Juventus kama kushinda mataji kadhaa ya Serie A, Copa Italia, vilevile kucheza fainali mbili za Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Lakini pia beki huyo amefanikiwa kwenye ngazi ya timu ya taifa kwa kutwaa taji la Euro mwaka 2021 akiwa na Italia.