Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Leo tutaiona ile Mamelodi yenyewe - Dauda

Yangaaaa X Mamelodi Mamelodi Sundowns

Fri, 5 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sitegemei surprise yoyote ile kwa sababu kwenye mchezo wa kwanza kama wachezaji muhimu kwenye kikosi cha Yanga wangekuwa fit basi kwa namna yoyote hutegemei kama kocha angepanga kikosi bila Yao, Aucho au Pacome.

Kwakuwa wachezaji wote hao walikuwa na majeraha kulikuwa hakuna namna, ilibidi kutumia njia mbadala ya kuwatumia wachezaji ambao wako tayari kwa ajili ya mchezo husika.

Kwa namna nilivyoangalia mazoezi ya jana, sitarajii kumuona Pacome wala Yao kikosini. Pacome bado alikuwa anafanya mazoezi ya peke yake chini ya uangalizi wa mtaalam wa viungo, Yao alikuwa jukwaani kabisa.

Aucho yeye aliungana na wachezaji wengine kwenye mazoezi ya mwisho, bila shaka anaweza kuwa sehemu ya kikosi cha leo.

Mchezo wa kwanza Yanga iliwakosa wachezaji watatu wa kikosi cha kwanza, kocha alilazimika kutumia wachezaji wengine na kubadili mfumo wa uchezaji kulingana na aina ya wachezaji aliokuwanao. Wakacheza kwa nidhamu na kuwaheshimu Mamelodi.

Watu wanapaswa kuelewa pia hata Mamelodi walicheza kwa nidhamu kubwa na kwa kuwaheshimu Yanga, lakini mchezo wa leo utakuwa tofauti kabisa.

Mameloi wakiwa nyumbani watacheza kwa kasi kubwa na kushambulia sana hivyo tutegemeee kuiona Mamelodi ambayo ni Mabingwa wa AFL na wanafainali wa Champions League.

Kwa hiyo ili Yanga waweze kukabiliana na Mamelodi nafikiri wanapaswa kuwa na wachezaji wa kushambulia na sio kujilinda.

Mwisho kabisa nawapa nafasi kubwa Mamelodi Sundowns nafasi kubwa ya kupata matokeo kwenye mchezo wa leo na kuingia hatua ya Nusu Fainali hasa kutokana na kurejea kikosini kwa nahodha wao Themba Zwane.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live