Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Leo ni usiku wa wababe Afrika

Al Ahly X ES Tunis Leo ni usiku wa wababe Afrika

Sat, 18 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Leo kutakuwa na kivumbi haswa wakati ambapo mabingwa wa kihistoria kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Al Ahly watavaana na Espérance de Tunis kwenye fainali.

Hii ni fainali ya kwanza ya michuano hiyo mikubwa Afrika ambapo  Al Ahly kwenye mchezo huu itaanzia ugenini kwenye Uwanja wa Olympique de Rades.

Timu zote mbili zina rekodi kubwa kwenye michuano ya msimu huu huku Ahly ikiwa inatakwenda kutafuta ubingwa wa 13 na Espérance wanatafuta watano.

Mchezo huu unatajwa kuwa ndiyo mechi ambayo inakutanisha timu ambazo zimefika fainali ya michuano hii mara nyingi.

Es Tunis imefanikiwa kufika fainali mara nane, huku Al Ahly ikifika mara 14 kukiwa hakuna timu ambayo inazikaribia.

Mechi ya makipa:

Pamoja na ukubwa wa mchezo huu lakini makipa wa timu zote wanapewa nafasi kubwa ya kuuteka mchezo huu.

Makipa wote ni wadogo na hizi ni fainali zao za kwanza, Esperance watakuwa na kipa mwenye miaka 20 Amanallah Memmiche, huku Al Ahly wakitegemea langoni atakaa  Mostafa Shobeir mwenye miaka 24.

Memmiche, huu ni msimu wake wa pili na Watunisia hao, lakini ameshaonyesha kiwango cha juu kwenye michezo iliyopita ya ligi hiyo na yupo tayari kuhakikisha anaipa timu hiyo ushindi huu muhimu leo.

Kiwango chake kimeifanya timu yake kucheza michezo tisa mfululizo bila  kuruhusu bao kuanzia Desemba mwaka jana.

Kwa upande wa pili, Shobeir amekuwa na kiwango cha kutisha naye tangu alipoanza kukaa langoni baada ya nahodha wa Ahly, Mohamed El Shenawy kuwa nje ya uwanja.

Kipa huyo amefanikiwa kucheza michezo sita bila kuruhusu bao akiwa anafuata nyayo za baba yake Ahmed Shobeir ambaye aliwahi kuitumikia timu hiyo.

Dondoo za mechi:

1. Al Ahly inakwenda kwenye fainali ya sita kati ya saba za michuano hiyo za hivi karibuni, ambapo imeshinda tatu na kupoteza tatu ikiwemo ya msimu uliopita ambayo iliichapa  Wydad AC ya Morocco mabao 3-2.

2. ES Tunis inatafuta ubingwa wa kwanza wa michuano hiyo tangu mwaka 2019, ilipoichapa  Wydad AC na kutwaa ubingwa wa pili mfululizo.

3.Hii itakuwa mara ya nane  timu hizo zinakutana kuanzia mwaka 2018, Ahly imeshinda mara sita, Esperance mara moja na sare moja.

4 .Al Ahly haijapoteza kwenye michezo 18 ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa imeshinda 12 na kutoka sare michezo sita, ikiwa ni timu ya kwanza kucheza michezo mingi ya michuano hiyo bila kupoteza.

5 .Timu zote zinakwenda kwenye mchezo huu zikiwa zinatafuta rekodi ya kucheza michezo tisa mfululizo bila kuruhusu bao, huku ES Tunis ikipigiwa mashuti 78 mara ya mwisho kuruhusu ilikuwa dhidi ya  Al-Hilal Omdurman Desemba mwaka jana, Al Ahly imepigiwa mashuti 106 ambapo mara ya mwisho iliruhusu ilipovaana na Yanga Desemba mwaka jana.

6. Kiungo wa ES Tunis, Yan Sasse amehusika kwenye mabao manne kwenye michuano hiyo msimu huu amefunga matatu na kutoa pasi moja ya bao. Amezidiwa na staa wa zamani ASEC Mimosas’ Sankara Karamoko mwenye matano.

7 .Kipa wa Al Ahly, Mostafa Shobeir hajaruhusu bao lolote kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu huu  akiwa ameokoa michomo 28.

8. Wakati Ahly ikiwa inasubiri kulitetea kombe lake, Espérance Sportive de Tunis yenyewe inataka kumaliza ukame wa miaka mitano wa kuchukua kombe hilo ambapo ililitwaa kwa mara ya mwisho mwaka 2019.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live