Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Leo ni nusu fainali za kibabe AFCON

Nusu Fc Leo ni nusu fainali za kibabe AFCON

Wed, 7 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nusu fainali ya michuano ya 34 ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) inapigwa leo huko Ivory Coast.

Nigeria iliyotwaa taji hilo mwaka 1980, 1994 na 2013 itaikabili Afrika Kusini iliyoshinda 1996 kwenye uwanja wa Stade Alassane Ouattara uliopo Kaskazini mwa jiji la Abidjan.

Katika nusu fainali ya pili wenyeji Ivory Coast waliotwaa kombe hilo mwaka 1992 na 2015 itachuana na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo iliyokuwa bingwa mwaka 1968 na 1974 kwenye uwanja wa La Paix uliopo jiji la Bouaké.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live