Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Leo ndio leo Uchaguzi Bodi ya Ligi

Uchaguzi Bodi Ya Ligi Taarifa ya Kamati ya Uchaguzi

Fri, 3 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uchaguzi wa Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TPLB) sasa utafanyika leo katika hoteli ya Cate mjini Morogoro.

Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Kiomoni Kibamba imesema kwamba uchaguzi utatanguliwa na Mkutano wa Baraza Kuu la TPLB Saa 3:00 asubuhi.

Mwenyekiti wa sasa Bodi, Steven Jarvis Mnguto wa Coastal Union ndiye mgombea pekee aliyepitishwa kuwania tena nafasi hiyo baada ya kuenguliwa Mwenyekiti wa Yanga SC, Dk Mshindo Mbette Msolla na wa Simba SC, Murtaza Ally Mangungu, huku Mwenyekiti wa Azam FC, Nassor Idrisa ‘Father’ pekee akipitishwa kugombea nafasi ya Makamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live