Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Leo ndio Leo mshindi wa tuzo ya Ballon D'or

Ballon D'or Tuzo hii itatolewa leo Novemba 29

Mon, 29 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Usiku wa leo itatolewa Tuzo ya Ballon D'or na mshindi atatangazwa baada ya kuwa siku hii imesubiriwa kwa muda mrefu.

Tuzo hiyo itatolewa nchini Ufaransa usiku wa leo katika Jiji la Paris baada ya kukosekana mwaka uliopita kutokana na kuzuka kwa janga la virusi vya Corona.

Lionel Messi ndie mchezaji anaepigiwa upatu kunyakua tuzo hiyo kwa upande wa wanaume huku akitarajiwa kuandika rekodi mpya lkwa kuinyakua tuzo hiyo kwa mara ya saba.

Mshambuliaji huyo wa PSG alimaliza ukame wake wa kushinda Kombe na timu ya Taifa baada ya kuisaidia Argentina kushinda ubingwa wa Kombe la Copa America kabla ya kuisaidia Barcelona kushinda kokombe cha mfalme kisha akatimkia PSG mwezi August kwa uhamisho huru.

Mpinzani wa karibu wa Messi katika kinyang'anyiro hicho ni fowadi wa Poland na Bayern Munich Robert Lewandowski, ambae alifanya vizuri mwaka 2020 kabla ya waandaaji wa tuzo hizo kusitisha kutokana na Janga la Covid-19.

Lewandowski amefunga magoli 73 katika michezo 60 akiwa na Bayern tangu kuanza kwa msimu uliopita na ameshinda Tuzo ya FIFA na UEFA kwa mwaka 2020, kwa upande wa wanaume.

Orodha ya wanaowania tuzo hiyo inajumlisha wachezaji 30 kutoka vilabu na mataifa mbali mbali kama ifuatavyo.

Cesar Azpilicueta (Chelsea), Nicolo Barella (Inter Milan), Karim Benzema (Real Madrid), Leonardo Bonucci (Juventus), Kevin De Bruyne (Manchester City), Giorgio Chiellini (Juventus), Cristiano Ronaldo (Manchester United), Ruben Dias (Manchester City), Gianluigi Donnarumma (Paris Saint-Germain), Bruno Fernandes (Manchester United), Phil Foden (Manchester City), Erling Haaland (Borussia Dortmund), Jorginho (Chelsea), Harry Kane (Tottenham), N'Golo Kante (Chelsea), Simon Kjaer (AC Milan), Robert Lewandowski (Bayern Munich), Romelu Lukaku (Chelsea), Riyad Mahrez (Manchester City), Lautaro Martinez (Inter Milan), Kylian Mbappe (Paris Saint-Germain), Lionel Messi (Paris Saint-Germain), Luka Modric (Real Madrid), Gerard Moreno (Villarreal), Mason Mount (Chelsea), Neymar (Paris Saint-Germain), Pedri (Barcelona), Mohamed Salah (Liverpool), Raheem Sterling (Manchester City), Luis Suarez (Atletico Madrid)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live