Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Leicester bingwa ngao ya Jamii

Kelech Ihenacho Mshambuliaji na mfungaji pekee wa goli la leicesrter,Kelechi Iheanacho

Sun, 8 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Leicester City imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Manchester City na hivyo kubeba kombe la Ngao ya Jamii.

Katika mchezo huo uliokuwa na upinzani wa hali ya juu ilibidi kusubiri mpaka dakika ya 88 kufugwa kwa bao pekee lililoamua mchezo huo.

Goli la Leicester limefungwa na kelechi Iheancho kwa mkwaju wa penati,dakika za mwisho kabisa mwa mchezo, na kuwaadhibu waajiri wake wa zamani.

Katika mchezo huo ambao umepigwa katika dimba la Wembley nchini Uingereza,ulikuwa kivutio cha wengi hasa baada ya kuingia kwa mchezaji ghali zaidi nchini Uingereza na ambae amesajiliwa hivi karibuni na manchester city ,Jack Grealish.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live