Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Legend Mamelodi: Yanga vs Mamelodi mechi ilikuwa ngumu sana

Kekana (1).jpeg Hlompho Kekana

Tue, 2 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Mamelodi Sundowns imepost mahojiano na legend wao mwenye mafanikio zaidi katika kikosi hicho, Hlompho Kekana kuhusu mechi yaoo ya kesho ya (Dstv) na mechi ya Yanga iliyopita na ijayo.

Katika mchezo wa awali wa robo fainali ya CAFCL, Yanga ilitoa sare ya bila kufungana na Mamelodi ambao ni mabingwa watetezi wa AFL.

"Yanga dhidi ya Mamelodi Sundowns ilikuwa mechi bora sana kimbinu kwa timu zote mbili japo kuna changamoto zake zilizotokea mpaka msafara wa Mamelodi ukachelewa kuingia uwanjani, nadhani ni kutokana na ukubwa wa timu, Mashabiki wamehamasika kwenda kuutazama mchezo huo.

"Kikawaida huwa ni ngumu sana kupambana na hisia za Mashabiki, itoshe kusema ilikuwa mechi nzuri sana," amesema Kekana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live