Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Leeds United wamtimua Kocha

Jesse Marsch .jpeg Jesse Marsch

Mon, 6 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Leeds United wamemfuta kazi kocha Jesse Marsch kufuatia kichapo cha kusikitisha cha 1-0 hapo jana dhidi ya Nottingham Forest ambao bado wanajitafuta EPL.

Taarifa ya klabu ilisema: “Tungependa kumshukuru Jesse na wasaidizi wake kwa juhudi zao na tunawatakia heri kwa siku zijazo. Mchakato wa kumteua kocha mkuu mpya unaendelea na tutaendelea kuwajulisha mashabiki katika siku zote zijazo.”

Marsch mwenye miaka 49, amedumu chini ya miezi 12 akiisimamia Elland Road baada ya kuteuliwa kama mrithi wa Marcelo Bielsa mwishoni mwa Februari mwaka jana.

Kocha huyo raia wa Marekani alii akisha Leeds kwenye Ligi ya EPL msimu wa 2021-22 lakini timu yake imekuwa ikifanya vibaya msimu huu licha ya kuungwa mkono kwa kiasi kikubwa katika soko la uhamisho.

Leeds imesajili wachezaji 10 wapya katika madirisha mawili ya uhamisho ya wachezaji, na watatu waliwasili Januari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live