Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Leeds United Wakumbana na Rungu la FA

Leedss.jpeg Leeds United

Tue, 21 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

FA, wamethibitisha kuwapiga faini klabu ya Leeds United kwa kushindwa kuwazui wachezaji wake kwenye mchezo ulioisha kwa kupoteza 3-2 dhidi ya Chelsea tarehe 11 Disemba.

Tukio lililopelekea klabu ya leeds kupatiwa adhabu ilikuwa penati ya dakika ya mwisho waliyozawadiwa klabu ya Chelsea kwenye muda wa nyiongeza ndani ya dimba la Stamford Bridge baada ya Klich kumchezea vibaya Rudiger na refarii kuomba msaada wa VAR kufanya maamuzi ya kuwazadia penati.

Msemaji wa FA alitoa waraka ambao ulionesha kuwa klabu ya leeds United imekubali kulipa faini ya Pauni 20,000 kwa kuvunja sheria kifungu cha 20.1.

“Leeds United wamekubali kuwa walishindwa kuwazuia wachezaji wao wenyewe kwa kufuatua utaratibu mzuri wa kiungwana pale walipomzunguka refarii na kumzonga na pia wamekubali adhabu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live