Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lazio kujaribu bahati yao kwa Greenwood

Mason Greenwood Brace Mason Greenwood

Fri, 21 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Lazio imeanza mazungumzo na Manchester United ili kuipata huduma ya mshambuliaji wa timu hiyo, Mason Greenwood, 22, ambaye imepanga kuwasilisha ofa ya Pauni 30 milioni ili kuipata saini yake.

Greenwood ambaye pia huduma yake inahitajika na Juventus na Napoli, mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2025. Msimu uliomalizika alicheza mechi 36 za michuano yote na kufunga mabao 10.

LIVERPOOL imepanga kuzipiku Chelsea na Manchester United kwa ajili ya kuipata saini ya winga wa Crystal Palace na Ufaransa Michael Olise, 22, dirisha hili. Taarifa za hivi karibuni zilieleza Chelsea imepanga kumuuza winga wao Mykhailo Mudryk ili kupata pesa itakazozitumia kumsajili Olise.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.

TOTTENHAM inaonekana kuwa kinara mbele ya Aston Villa katika mchakato wa kuiwania saini ya kiungo wa Juventus na Marekani, Weston McKennie, 25, dirisha hili.

Weston ilidaiwa kuwa kwenye mchakato wa kutua Villa kama sehemu ya mabadilishano ya dili la Douglas Luiz kutua Juventus ingawa Spurs nayo inataka kuonyesha jeuri yake kwa kuiwinda saini yake.

MABOSI wa Juventus wamefikia patamu katika mchakato wao wa kutaka kumsajili kiungo wa Aston Villa, Douglas Luiz na mchumba wake Alisha Lehmann dirisha hili.

Juventus inahitaji sana huduma ya Luiz na katika kufanikisha hilo imepanga kumtoa kiungo wao Samuel Iling-Junior, 20, kama sehemu ya ofa. Mkataba wa Luiz unamalizika mwaka 2026.

WINGA wa Athletic Bilbao, Nico Williams, 21, amewasisitiza wawakilishi wake anataka kujiunga na Barcelona licha ya kuwepo kwa timu nyingi za England zinazohitaji kumsajili.

Staa huyu wa kimataifa wa Hispania, huduma yake pia inawindwa na Aston Villa, Arsenal, Liverpool na Newcastle United. Mkataba wake unamalizika mwaka 2027.

INTER Milan imeingia vitani dhidi ya AC Milan ili kuipata saini ya beki wa kulia wa Aston Villa, Matty Cash, 26, dirisha hili ili akawe mbadala wa Danzel Dumfries anayetarajiwa kuondoka dirisha hili.

Inaelezewa Milan ilishatuma hadi wawakilishi wake England kukutana na mabosi wa Villa ili kuanza mazungumzo ya kumsajili Cash, lakini kuingia kwa Inter katika dili kunaweza kutia ugumu.

CHELSEA imemwongeza straika wa Atletico Madrid, Samu Omorodion kwenye orodha ya washambuliaji inayohitaji kuwasajili dirisha hili akiwamo Jhon Duran.

Omorodion amewavutia Chelsea kutokana na umri wake akiwa bado ana miaka 20 na kiwango alichoonyesha msimu uliopita alipokuwa kwa mkopo Alaves alikocheza mechi 36 za michuano yote na kufunga mabao tisa.

Chanzo: Mwanaspoti