Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lautaro Martinez atikisa kibiriti Inter Milan

Image 5 1140x640.png Lautaro Martinez atikisa kibiriti Inter Milan

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: Dar24

Mshambuliaji kutoka nchini Argentina Lautaro Martinez amewaambia mabosi wa klabu ya Inter Milan kwamba anataka kuondoka licha ya vigogo hao kumshawishi asaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia kwenye viunga vya mji wa Milan.

Martinez mwenye umri wa miaka 26, anataka kuondoka kwa sababu huduma yake inawindwa na timu nyingi barani Ulaya ikiwa ni pamoja na Chelsea na Real Madrid.

Nyota huyu wa kimataifa wa Argentina tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi saba za michuano yote akifunga mabao sita na kutoa asisti mbili, lakini mara zote amekuwa moto kweli kweli Uwanjani. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika ifikapo 2026.

Katika madirisha mawili yaliyopita mchezaji huyu aliwahi kuhusishwa kusakwa na FC Barcelona, lakini ilishindikana kumsajili.

Kocha wa Manchester United, Erik Ten Hag anaamini Mshambuliaji huyo akijiunga kwenye timu ataboresha zaidi eneo la ushambuliaji ambalo msimu huu limekuwa na changamoto nyingi.

Chanzo: Dar24