Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lasheen aligomea penalti ya Misri

Mohand Lasheen Egypt 2021 Lasheen aligomea penalti ya Misri

Tue, 30 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

KIUNGO Mohanad Lasheen, 27, ameripotiwa alikataa kupiga penalti ya tisa na ya mwisho ya Misri dhidi ya DR Congo, na hivyo kumlazimu kipa wao Mohamed Abou-Gabal kwenda kuipiga.

Misri imetolewa kwenye hatua ya 16-Bora ya fainali za Mataifa ya Afrika baada ya kulala kwa penalti 8-7 dhidi ya DR Congo.

Penalti ya mwisho ilipigwa na kipa Abou-Gabal ambaye aliishia kugongesha besela, kabla ya kipa wa DR Congo, Lionel Mpasi kufunga penalti ya ushindi.

Hata hivyo, beIN Sports inabainisha kuwa kiungo Lasheen, ambaye aliingia kutokea benchini dakika chache kabla ya kuanza kwa hatua ya kupigiana ‘matuta’, ndiye aliyepaswa kupiga penalti hiyo na sio Abou-Gabal, lakini alikataa.

Lasheen ndiye aliyekosa penalti ya mwisho ya Misri katika mechi ya fainali ya AFCON 2021 dhidi ya Senegal waliotwaa ubingwa, katika mechi ambayo pia aliingia ‘sub’ katika muda za ziada kama ilivyotokea juzi.

Chanzo: Mwanaspoti