Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Laporte kuondoka Man City mwishoni mwa msimu

Laporte Ay.jpeg Mlinzi wa Man City, Aymeric Laporte

Tue, 7 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa klabu ya Manchester City Aymeric Laporte anatarajia kutimka ndani ya klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu na vilabu mbalimbali vinatajwa kutaka saini ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania.

Laporte anaripotiwa mwishoni mwa msimu huu atatimka kwenye klabu ya Manchester City huku klabu ya Barcelona ikitajwa kwa kiwango kikubwa kua ndio yataenda kua makazi yake mapya, Lakini mpaka sasa klabu hiyo haijaweka wazi kua inamhitaji beki huyo.

Klabu ya Manchester City ipo kwenye hatari ya kukosa wachezaji wake wawili kwenda klabu ya Barcelona kama na beki huyo atajiunga na Barcelona, Kwani vinara hao wa ligi kuu nchini Hispania wamekua wakimuhitaji kiungo wa klabu hiyo Bernardo Silva ambaye alishaonesha nia ya kutaka kuondoka klabu hiyo mara tatu.

Klabu ya Manchester City imeshajiandaa kama beki Aymeric Laporte ataondoka klabuni hapo wao wamepanga kumnunua beki wa klabu ya Rb Leipzig raia wa kimataifa wa Croatia Josko Gvardiol ambaye amekua kwenye kiwango kikubwa ndani ya ligi kuu ya Ujerumani.

Laporte amekua kwenye kiwango kizuri ndani ya Manchester City kwa kipindi kirefu sasa lakini hivi karibuni amekua hana nafasi ya kudumu ndani ya klabu hiyo inaweza kua sababu ya mchezaji huyo kuamua kutafuta klabu nyingine ambayo atakua anapata nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live