Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lampard kulamba dili Rangers

Frank Lampard Rangers Badge Lampard kulamba dili Rangers

Sat, 7 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mujibu wa ripoti, klabu ya Rangers imefanya mazungumzo na Frank Lampard kwa ajili ya kuwa kocha wao. Klabu hiyo inasaka kocha mkuu baada ya kumfukuza Michael Beale wiki iliyopita kutokana na mwanzo mbaya msimu huu.

Steven Davis anaiogoza timu kwa sasa kama kocha wa mpito akisaidiwa na Alex Rae na walipokea kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Aris Limassol katika mechi ya Ligi ya Europa kwa mara ya kwanza tangu walipopewa timu.

Klabu hiyo imepania kuleta kocha mkuu achukue nafasi ya Beale aliyetimuliwa, kwa mujibu wa ripoti, huku mazungumzo kati ya Lampard yanaendelea vizuri ili kufikia makubaliano ya kuwa kocha mkuu.

Lampard, ambaye hajapata timu tangu alipoondoka Chelsea kwa mara ya pili kama kocha, imeelezwa alionana na mabosi wa Rangers Jumatano usiku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live