Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lampard haofii kibarua chake Everton

Frank Lampard Coach.jpeg Kocha wa Everton, Frank Lampard

Thu, 5 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa klabu ya Everton Frank Lampard amesema anajua kua klabu ya Everton inahitaji kupata matokeo ya ushindi lakini yeye hahitaji kuhakikishiwa kuendelea kuwepo kazini.

Baada ya kupoteza dhidi ya Brighton siku ya jumanne kwa magoli 4-1 kichapo ambacho kimefanya klabu hiyo kushuka chini na kufika kwenye timu tatu za mwisho kwenye msimamo wa ligi kuu ya EPL, Jambo ambalo linamuweka kocha huyo kwenye wakati mgumu.

Kocha Lampard ambaye alitangazwa kuchukua nafasi ya kocha Rafa Benitez mwezi Januari mwaka 2022, Amefanikiwa kushinda michezo tisa pekee kwenye michezo 36 ambayo ameisimamia klabu hiyo kutoka jiji la Liverpool.

Kocha huyo alifanikiwa kuiepusha klabu ya Everton kushuka daraja msimu uliomalizika baada ya kupata matokeo ya ushindi katika michezo ya mwisho ya ligi hiyo, Ikielezwa kua ndio sababu ya klabu hiyo kumuacha kocha huyo mpaka sasa licha ya matokeo mabaya ambayo klabu hiyo inaendelea kuvuna.

Frank Lampard ameeleza yeye yupo kuhakikisha kua timu hiyo inafanya vizuri na kushinda michezo ambayo ipo mbele yao, Lakini hahitaji kuhakikishiwa usalama wa ajira yake siku za mbeleni na lengo lake kubwa ni kuhakikisha klabu hiyo inabaki kwenye ligi kuu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live