Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lampard awapa onyo Chelsea

Frank Lampard 1140x640 Frank Lampard

Sun, 9 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Gwiji wa Chelsea, Frank Lampard ametoa onyo kwa klabu yake hiyo ya zamani akiwataka kuacha mtindo wao wa kubadili makocha kila wakati.

Kocha huyo wa zamani wa Derby, Chelsea na Everton, Lampard ametaka mabosi wa klabu hiyo ya Stamford Bridge wanapaswa kuwa wavumilivu kwa makocha wao wanaowaajiri na kuwapa kazi ya kuinoa timu hiyo.

Kiungo huyo wa zamani wa kimataifa wa England, Lampard alisema kitendo cha Chelsea kumpa kazi Enzo Maresca, ambaye wamemchukua kutoka Leicester City ni ishara kwamba imelenga mafanikio ya muda mrefu, hivyo wanapaswa kuwa na imani na kuvumilia makocha wao.

Akizungumza na talkSPORT, gwiji huyo wa The Blues alisema: “Ilikuwa jambo zuri kuona mwisho mzuri wa msimu kwenye ligi iliyopita.

“Nilikuwa kwenye benchi la ufundi la ile timu misimu ya huko nyuma, najua kinachoendelea kuna ugumu sana. Kule klabu inataka kwenda na mahali ilipo kwa sasa, kuna pengo kubwa sana baina yao na klabu za kiwango cha juu.

“Bado kuna pengo kubwa, hivyo nadhani kunahitajika uvumilivu wa hali ya juu kumpa kocha mpya nafasi ya kufanya kazi, kutazama kikosi chake, kukiandaa ili kila mchezaji anayekuja kwenye timu awe na mchango.

“Ngoja tuone itakavyokuwa msimu ujoa, kama watamaliza vizuri basi itakuwa kitu kizuri. Tusubiri mwanzo wa msimu utakavyokuwa.”

Chanzo: Mwanaspoti