Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lampard asikitikiwa kila kona

Frank Lampard 1140x640 Frank Lampard

Tue, 11 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkongwe wa Arsenal, Ian Wright amemuonea huruma Frank Lampard baada ya kurejea Chelsea akiwa kama kocha wa muda.

Lampard aliteuliwa kuwa kocha muda wa Chelsea hadi msimu utakapomalizika baada ya Graham Potter kufukuzwa kazi.

Hata hivyo Lampard alianza vibaya na akashuhudia kikosi chake kikipokea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Wolves, kwenye mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu England.

Lakini mkongwe huyo wa Arsenal akamsikitia Lampard akidai hakuona sababu ya kurudi Stamford Bridge baada ya kufukuzwa kazi mwaka 2021.

Umekuwa msimu mbovu kwa Chelsea ambayo ipo nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi ikiachwa pointi 17 dhidi ya timu nne za juu, licha ya Todd Boehly kutumia Pauni 600 milioni kwenye usajili wa dirisha la usajili la kiangazi.

Akizungmza kupitia cha televisheni cha BBC, Wright alisema anaogopa kushuhudia kitachomtokea Lampard katika mechi za ligi zilizobaki.

"Naogopa sana, nachotaka Lampard afanye vizuri, nadhani hakuwa muda sahihi kwake kurudi Chelsea, lakini kupewa ajira katika klabu hiyo sio jambo dogo, lakini namuonea huruma kama rafiki yangu, je itamsidia? au amerudi kwasababu maalumu? au anataka kurejea kazi yake ya ukocha? imenichanganya sana na napata mashata kuhusu hata yote," alisema Wright

Lampard alikuwa na siku mbili tu kukikagua kikosi cha Chelsea, kabla ya kumenyana na Wolves kwenye mechi yake ya kwanza ya ligi baada ya kuteuliwa kuwa kocha wa muda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live