Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lampard achafua hali ya hewa Chelsea

Lampard Vs Brighton.jpeg Lampard achafua hali ya hewa Chelsea

Thu, 20 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unaweza kusema kocha wa mpito wa Chelsea Frank Lampard ni kama amekosa bahati tangu arejeshwe kukinoa kikosi hicho.

Chelsea imepoteza tumaini jingine la kunyenyua makwapa angalau kwa kombe moja msimu huu baada ya kuwa nje ya mbio za ubingwa EPL, Carabao, FA Cup kwani mpaka sasa wapo nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Premier League.

Baada ya kuondoshwa kwenye UEFA Champions League kwa jumla ya mabao 4-0, ambapo Real Madrid walifanikiwa kuwafunga vijana wa Lampard nje ndani kwa mabao 2 kila raundi.

Lampard aliletwa na Chelsea baada ya kutimuliwa Graham Potter, lakini kwa sasa amefikia rekodi isiyotakikana klabuni hapo ambapo alikuwa gwiji na kiungo wa mabao.

Ukiwa na meridianbet unaweza kubashiri mubashara, tembelea maduka ya meridianbet uweze kucheza michezo ya sloti na kasino ya mtandaoni.

Ndiye meneja wa kwanza kabisa wa The Blues kuonja kichapo katika mechi zake zote nne za kwanza akiwa kama kocha tangu arudi klabuni hapo, huku akiwa meneja ameandikisha ushindi mmoja katika michezo yake 18 iliyopita.

Rekodi hiyo kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii ni dhuluma kidogo ikizingatiwa kuwa alikuwa akisimamia hatari ya kushuka daraja wakati akiwa na Everton.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: