Mon, 31 Jan 2022
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Klabu ya Everton sasa ni rasmi imemteua Frank Lampard kuwa Kocha mpya akichukua mikoba ya mtangulizi wake Rafa Benitez alietimuliwa wiki chache zilizopita.
Everton kwa sasa inakamata nafasi ya 16 katika msimamo wa Ligi ilimtimua Benitez baada ya kipigo cha magoli 2-1 kutoka kwa Norwich.
Lampard amesaini mkataba wa miaka miwili na nusu katika klabu hiyo iliyopo mji wa merseyside utakaoisha 2024.
Kibarua cha Kwanza cha Lampard kinatarajiwa kuwa katika kombe la FA, mchezo wa raundi ya nne dhidi ya Brentford katika uwanja wa Goodison Park siku ya Jumamosi.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live