Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lampard, Dean Smith nani kupewa dhamana Norwich City ?

Frank Lampard Aliyekuwa Meneja wa Chelsea, Frank Lampard

Fri, 12 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aston Villa, Watford na Newcastle United wameshaamua makocha wapya. Norwich City bado hakijaeleweka ni Frank Lampard vs Dean Smith.

Vilabu vinne kati ya vitano vinavyoshikilia nafasi za mwishoni kwenye msimamo wa EPL, vimeamua kuchukua hatua za haraka kubadilisha upepo. Makocha wa vilabu hivyo wameoneshwa milango ya kutokea na kupisha wengine kuchukua nafasi.

Kati ya vilabu vinne, ni Norwich City pekee ambayo bado haijaamua mrithi wa Daniel Farke ni nani? Wengi wamehusishwa lakini mpaka sasa – ni mbio za mafahali wawili.

Tangu atimuliwe Chelsea na nafasi yake kupewa Thomas Tuchel kuelekea mwishoni mwa msimu uliopita, Frank Lampard hajapata kazi mpaka sasa. Uwepo wa nafasi pale Carrow Road ni fursa kwa Lampard na uongozi wa klabu hiyo.

Lampard anatajwa kama kocha mwenye sifa na weledi mkubwa wa uongozi. Pamoja na hilo, uongozi wa klabu hiyo unamuona Lampard kama mtu sahihi atakayeweza kuwavutia wachezaji kujiunga na klabu hiyo.

Upande wa pili kuna Dean Smith. Japokuwa ametimuliwa Aston Villa, Smith anatajwa kama kocha aliyewavutia zaidi viongozi wa Norwich City wakati wa mazungumzo yao. Uzoefu wa Smith kwenye EPL na Championship ni vitu vikubwa ambavyo vinamtofautisha yeye na Lampard.

Mpaka sasa, sio Lampard wala Smith aliyethibitisha kuchukua mikoba ya Daniel Farke. Lakini, kuelekea kurejea kwa EPL wikiendi ijayo, lolote linaweza kutokea kwa siku za usoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live