Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lamine Yamal na demu wake pachimbika

Lamine Yamal Ewd Lamine Yamal.

Tue, 30 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Inaonekana kuna mdudu mbaya ameingia ndani ya nyumba kwa sababu siku chache tu tangu kujitokeza hadharani kuwa wako katika uhusiano, staa wa Hispania na Barcelona, Lamine Yamal na kimwana Alexandra Padilla kila mmoja amem-unfollow mwenzake Instagram.

Jambo hilo limekuja baada ya Alexandra kuonekana akikaa mapajani mwa mwanaume mwingine ‘live’ kupitia ukurasa wa TikTok.

Video ya tukio hilo ambayo tayari imepata umaarufu mkubwa, inaanza kwa vijana wakifurahi pamoja, huku Yamal akiwa haonekani popote, jambo lililovuta macho ya watu kutaka kujua kulikoni.

Hata hivyo, sekunde chache baadaye mmoja wa marafiki wa binti huyo akaelekezea kamera alipo mwanadada huyo, ambako alidaiwa kukaa kwenye mapaja ya mwanaume mwingine.

Baada ya kustukia kwamba kamera inamuonyesha ‘live’ katika jambo hilo, haraka akaipiga kofi skrini ya simu iliyokuwa ikimrekodi na kumponyoka mkononi anayerekodi, kabla ya ‘live’ hiyo kufikia tamati sekunde chache baadaye.

Baada ya mashabiki kuiona video hiyo, Lamine na mwanadada huyo ambaye ni mwanafunzi na pia mwenyeji wa mji wa Barcelona, kila mmoja akam-unfollow mwenzake kwenye kurasa zao za Instagram.

Kumbuka kwamba tangu Yamal na Padilla walipojitambulisha hadharani, akaunti ya mwanadada huyo imeongezeka haraka wafuasi na kufikia milioni 1.6 kwenye TikTok, wakati akaunti yake mpya ya Instagram ilivuna zaidi ya wafuasi 420,000 ndani ya siku 7 tu tangu ianzishwe.

Iliripotiwa mapema kwamba wawili hao wangepanda ndege kwenda kula bata la mapumziko huko Kos Island, ambako wangeenda kuendesha boti pamoja. Hata hivyo, hakuna kati yao aliyeposti picha katika ‘Insta story’ zao wakiwa pamoja.

Na sasa maswali yameibuka kuhusu hatima ya uhusiano wa wawili hao, huku mashabiki wakidai kwamba wawili hao wameshamwagana. Kama ni kweli, uhusiano wao utaingia katika historia ya uhusiano uliodumu kwa muda mfupi zaidi, ukidumu kwa chini ya miezi minne tu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live