Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lakers yalala mbele Milwaukee Bucks

Los Angeles Lakers Los Angeles Lakers.

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya kikapu ya Milwaukee Bucks imewalaza Los Angeles Lakers kwa alama 108 dhidi ya alama 97 kwenye mchezo wa maandalizi ya msimu mpya wa ligi ya kikapu nchini Marekani 2023-24 uliochezwa usiku wa Jumapili ya Oktoba 15-2023.

Nyota mpya wa Bucks Damian Lillard alifunga alama 14 na kutoa pasi za usaidizi wa magoli mara 3 huku Giannis Antetokounmpo akifunga alama 16 huku upande wa lakers Anthony Davis akifunga alama 16 ilhali kwenye mchezo huo Lakers ilikosa huduma ya nyota wao LeBron James.

Msimu mpya wa Ligi ya kikapu ya Marekani NBA 2023-24 ambao utakuwa ni makala ya 78 tangu kuanzishwa kwa ligi ya kikapu nchini Marekani unataraji kuanza Jumanne ya Oktoba 24-2023 na kutaraji kuhitimishwa Jumapili ya Aprili 14-2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live