Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

LIVE KUTOKA RUANGWA: Mayele aliamsha Yanga

Mayele Mtwara Fiston Mayele

Wed, 7 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele amerejea kwenye kikosi cha timu hiyo kufanya mazoezi ya pamoja wakijiandaa na mchezo wa kesho dhidi ya Namungo.

Mayele alikosekana kwenye mchezo uliopita dhidi ya Tanzania Prisons baada ya kuelezwa ana majeraha madogo.

Mshambuliaji huyo kwenye mazoezi yanayoendelea hapa kwenye uwanja wa Majaliwa alionekana kuchechemea kwa mbali lakini haikumfanya ashindwe kufanya mazoezi na wenzake.

Namungo na Yanga zitacheza kesho saa 1:00 usiku katika uwanja wa Majaliwa ikiwa ni mechi ya mwisho kwa timu hizo kumaliza mzunguko wa kwanza kwenye ligi.

Wachezaji waliokuwa kwenye mazoezi hayo ni Djuma Shaban, Yanick Bangala, Clement Mzize, Zawadi Mauya, Bernard Morrison, Tuisila Kisinda, Joyce Lomalisa na Jesus Moloko.

Wengine ni Ibrahim Bacca, Dickson Job, Dicksom Ambundo, Khalid Aucho, Feisal Salum, Gael Bigirimana, Denis Nkane, Aziz Ki,David Bryson, Djigui Diara na Eric Johora.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live