Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kweli Yanga watoe sh milioni 216 sababu ya Okrah?

Okrah Mtineeeeee Okrah Magic

Wed, 21 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Lazima umeisikia taarifa ya kuwa Shirikisho la Soka la Kimataifa( Fifa) limeitaka klabu ya Yanga kuilipa klabu ya Bechem United ya Ghana kiasi cha dola za Kimarekani 80,000 sawa na Tsh Milioni 216 ndani ya siku 45 kuanzia sasa ikiwa ni pesa ya malipo iliyosalia katika uhamisho wa Augustine Okrah kutoka Bechem United kwenda Yanga.

Kwangu naona hii si sawa Yanga kuendelea kuingia kwenye madeni kupitia wachezaji wa FURAHISHA GENGE.

Najua itakuwa vigumu watu kuelewa kwa kuwa Yanga sasa wanashinda na wako vizuri lakini madeni kama haya na yale ya akina Bigirimana YANABAKI kwenye klabu na YANGEWEZA KUEPUKIKA.

Ukiangalia usajili wao inakuwa si kukosea lakini ni kama SIASA hivi au kutaka kuonyeshana hivi.

Najua taarifa inasema Yanga wanapaswa kuwa wamekubali au kupinga mpaka ifikapo tarehe 3 Septemba 2024 vinginevyo baada ya tarehe hiyo itachukuliwa kuwa wamekubali KULIKO KUFIKA HUKU HAYA YANAEPUKIKA...

Okrah kweli... anyway... kuna haja ya kuzipunguzia MZIGO WA MADENI KLABU ZETU kwa kuongeza umakini kwenye usajili na kuufanya usajili uwe kwa MANUFAA YA KLABU.

Saleh Jembe

Chanzo: www.tanzaniaweb.live