Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kweli Balua ni bora kuliko Kibu?

Balua Simba Sz Kweli Balua ni bora kuliko Kibu?

Wed, 8 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuna radio moja nchini (X) nilikuwa naisikiliza asubuhi ya leo hii, kuna Mchambuzi mwenzangu anasema Edwin Balua ni Product zaidi kuliko Kibu Denis aiseee nilizima radio faster sana, I think watu wamekuwa hawana hata "Respect " na kazi anayoifanya Kibu daah, hii imeniuma hata kama huwa siingii uwanjani

Watu wanamcount kwasababu ya goli moja na sio utandaji wake daah, lakini kuhusu masuala mbalimbali uwanjani hawazungumzi: Kibu amekuwa anaweka presha kwa mpinzani na kujikuta mpinzani build up yake inakosa utulivu (offensive), akiwa na mpira uuchukua kwake ni ngumu unless umfanyie fouls huwa ni faida ya timu kupata set pieces.

Akipoteza mpira akiwa juu sana huwa ana uwezo wa kukabia juu (counter pressing) ili kuurudisha mpira kwa timu (defensive), anakupa faida kwenye phase zote 3 muhimu uwanjani licha ya finishing yake kuwa chini lakini anakupa faida fouls, pressing, crossing, pass and penalties: jukumu la kuzuia ni la timu nzima basi Kibu atakupa wastani huo, sio abiria kama baadhi ya Wachezaji wenzake.

Makocha wengi wamekuwa wakimtumia Kibu Denis wakijua anakupa vitu vingi zaidi na sio lazima ufunge (Robertinho, Mgunda, Pablo, Benchikha etc ), unafikiri walikuwa hawaoni anachokionesha mazoezini? Au walikuwa walikuwa wanalazimishwa kumpanga wengine hawapo? So Balua hawezi kufika hata 70% ya products anazozitoa Kibu Denis.

Sitaki kumpinga Mchambuzi mwenzangu kutoka radio (X) kwasababu kila mtu ana namna yake ya kuuangalia mpira na wengine hawariziki, na sitaki kuwapinga lakini nimeona kama ni disrespect kwa Kibu Denis, inaonekana Kibu kutafuta thamani yake watu wameona ni kumdondoshea jumba bovu, bahati mbaya sana analipa gharama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live